Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwajulisha watu wote wanaotarajia kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) mwezi Mei 2025 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba Usajili wa Watahiniwa wa Kujitegemea Kidato cha Sita 2025 NECTA;
- Kipindi cha kawaida cha usajili wa Watahiniwa wa Kujitegemea kitakuwa kuanzia tarehe 01 Julai hadi 30 Septemba, 2024 kwa ada ya Shilingi 50,000/=. Aidha, watakaojisajili kwa kuchelewa yaani kuanzia tarehe 01 Oktoba hadi 31 Oktoba, 2024 watalipa Shilingi 65,000/= na hakutakuwa na usajili mwingine baada ya tarehe 31 Octoba 2024.
- Usajili utafanyika kwa njia ya mtandao (online). Aidha, kabla ya kujisajili, waombaji wanapaswa kwenda kwenye Vituo vya Mitihani kuchukua Namba Rejea (Reference Number) zinazotolewa bure na kufanya malipo ya ada kupitia Benki kwa kutumia ‘Control Number’.
- Ufafanuzi kuhusu utaratibu na hatua za kufuata katika kutengeneza ‘Control Number’ na kujisajili, umetolewa katika tovuti ya Baraza la Mitihani la Tanzania na kwa Wakuu wa Vituo vya Watahiniwa wa kujitegemea
Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwani mfumo wa usajili utafungwa baada ya kipindi cha usajili kukamilika.
Maelezo zaidi kuhusu usajili wa watahiniwa kidato cha sita 2025 soma hapa.
Soma zaidi: Jinsi ya kuangalia matokeo ya kidato cha sita 2024-25 NECTA
Leave a comment