Je, unatafuta kazi yenye changamoto na inayokidhi ndoto zako? Wilaya ya Hai ina Nafasi za kazi Wilaya ya Hai – Julai 2024 – Ajira Mpya Hai! Fursa hizi zimeundwa mahsusi kwa ajili yako, zikiwa na malengo ya kuinua viwango vya maisha na maendeleo katika jamii yetu. Sasa ni wakati wako wa kuchukua hatua na kujipatia nafasi ya kipekee ya kazi. Angalia nafasi hizi na ujiunge na timu yetu ili tuijenge Wilaya ya Hai pamoja.
Ajira Portal chaneli | Jiunge hapa |
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai kupitia kibali cha Ajira Mpya chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 chenye kada ya Mtendaji wa Kijiji Daraja la III nafasi kumi na tatu (13) na Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II nafasi tano (05) kilichotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, anawatangazia nafasi za kazi watanzania wenye sifa na ujuzi kwa nafasi zifuatazo:-
Mafasi zilizo Tangazwa
1. Mtendaji wa Kijiji – Nafasi 13
Sifa:
Awe na elimu ya kidato cha nne (iv) au sita (vi) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo:- Utawala, Sheria, Elimu ya jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka katika Chuo cha Serikali za Mitaa au chuo chochote kinachotambulika na Serikali.
Jinsi ya kutuma Maombi
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kieletroniki wa Ajira kupitia anwani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/advert/index (anwani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa (Recruitment Portal). Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 22 Julai, 2024.
Leave a comment