Wilaya ya Mvomero inakukaribisha kuomba Nafasi za kazi Wilaya ya Mvomero – Julai 2024 – Ajira Mpya Mvomero kutoka Utumishi. Hii ni fursa adhimu kwa wale wenye nia ya kutumikia jamii na kujenga mustakabali bora. Nafasi hizi zinalenga kuboresha huduma kwa wananchi. Usikose nafasi hii ya kipekee ya kuwa sehemu ya mabadiliko chanya katika Wilaya ya Mvomero. Tafuta kazi inayokidhi ndoto zako na ujenge taifa letu kwa pamoja!
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024. Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-
Ajira Portal chaneli | Jiunge hapa |
Nafasi zilizo Tangazwa
1. Dereva – Nafasi 5
- Sifa: Awe amehitimu kidato cha nne (IV) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV). Awe na leseni daraja ‘C’ au “E” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali, Awe amehudhuria JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MVOMERO Halmashauri ya Wilaya Mvomero, S.L.P. 663, Morogoro, Simu: +255232934348, Nukushi: +2552334348, Barua pepe: ded@mvomerodc.go.tz, tovuti: http://www.mvomerodc.go.tz mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
2. Mwandishi Mwendesha Ofisi – Nafasi 3
- Sifa: Kuajiriwa mhitimu wa Kidato cha IV au Kidato cha VI wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na serikali. Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
3. Msaidizi wa Kumbukumbu – Nafasi 3
- Sifa: Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) aliyehitimu Stashahada (NTA level 6) katika fani ya Masijala kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.
4. Mtendaji wa Kijiji – Nafasi 7
- Sifa: Mwombaji awe na Cheti cha kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo Cha Serikali za Mitaa au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
Jinsi ya kutuma Maombi
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kieletroniki wa Ajira kupitia anwani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/advert/index (anwani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa (Recruitment Portal). Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 23 Julai, 2024.
Leave a comment