“Karibu kwenye orodha ya Nafasi za kazi Jiji la Dodoma – Julai 2024 – Ajira Mpya Dodoma! Kama wewe unatafuta fursa mpya za ajira katika mji huu mkuu wa Tanzania kutoka Utumishi, hapa ndipo pa kuangalia. Tunakuletea orodha kamili ya nafasi za kazi zilizotangazwa hivi karibuni, zinazojumuisha fursa mbalimbali za kazi kulingana na ujuzi na taaluma yako. Endelea kusoma ili kujua zaidi na kujiandaa kupiga hatua mpya katika kazi yako!”
Miaka mingi iliyopita mji huu ambao unaitwa Dodoma ulikuwa ukifahamika kama Calangu (Chalangu) mji huu haukuwa na wenyeji bali ulikuwa na wahamiaji toka maeneo mengine ambao ni wamanghala, wabambali, wayenzele na wanghulimba. Wahamiaji hawa walikuwa wakitofautiana kwa tabia zao, wamanghala na wabambali waliishi msituni na walikuwa wawindaji wakila nyama na asali.
Ajira Portal chaneli | Jiunge hapa |
Soma:
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma amepokea Kibali cha Ajra mpya kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia barua yenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 ya tarehe 25.06.2024. Hivyo, anawatangazia wananchi wote wenye sifa kuomba nafasi mbalimbali za kazi. Nafasi husika ni kama zifuatavyo; –
Nafasi zilizo Tangazwa
1. Msaidizi wa Kumbukumbu – Nafasi 4
2. Mtendaji wa Mtaa – Nafasi 10
3. Mwandishi Mwendesha Ofisi – Nafasi 4
4. Dereva Daraja la II – Nafasi 4
Jinsi ya kutuma Maombi
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kieletroniki wa Ajira kupitia anwani ifuatayo; Bonyeza Hapa (anwani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa (Recruitment Portal). Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 25 Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa na ielekezwe kwa anuani ifuatayo: –
Mkurugenzi wa Jiji,
Halmashauri ya Jiji la Dodoma,
1 Mtaa wa CDA,
S.L.P. 1249,
DODOMA.
Leave a comment