Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga amepokea Kibali cha Ajira Mpya
kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora kupitia barua yenye Kumb.Na.FA. 97/288/01/09 ya tarehe 25 Juni, 2024. Hivyo;
anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa watanzania wenye sifa za kujaza nafasi
zifuatazo;-
Nafasi za kazi shinyanga
Share
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II NAFASI (4)
DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 05)
MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III (NAFASI 15)
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18
na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
i. Waombaji wawasilishe maelezo binafsi (Curriculum Vitae) yanayojitosheleza
(Detailed CV) yenye Anuani na Namba za simu za kuaminika pamoja na majina
ya wadhamini watatu (Referees) wa kuaminika.
ii. Waombaji waambatanishe nakala za vyeti vya Kidato cha Nne au Sita, Taaluma
na cheti cha kuzaliwa. Waombaji watakaowasilisha” Result Slip”,” Statement of
Results”,” Provisional Results” au” Transcripts HAVITAKUBALIKA.
Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 25 Julai, 2024.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana
kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa
‘Recruitment Portal’).