Leo kutoka INEC (NEC), Orodha ya Majina ya Walioitwa kwenye Usaili NEC – Muleba INEC Julai 2024; Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Muleba Kaskazini na Kusini anapenda kuwataarifu waombaji wote walioomba kazi ya Waandikishi Wasaidizi na Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki kuwa usaili unatarajia kuendeshwa kwa utaratibu ufuatao:-
- Wasailiwa wanaotoka katika Tarafa ya Nshamba na Muleba usaili utafanyika tarehe 22/07/2024 katika ukumbi wa Igabiro Farm (Chuo cha Kilimo) kuanzia saa 1:30 asubuhi.
- Wasailiwa wanaotoka katika Tarafa ya Kamachumu na Izigo usaili utafanyika tarehe 23/07/2024 katika ukumbi wa Shule ya Msingi St. Michael (Kagondo) kuanzia saa 1:30 asubuhi.
Wasailiwa wanaotoka katika Tarafa ya Kimwani usaili utafanyika tarehe 24/07/2024 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Kishoju kuanzia saa 1:30 asubuhi.
Bonyeza hapa kudownload majina ya walioitwa kwenye usaili NEC Muleba
Endelea kusoma maelezo zaidi chini…
Orodha ya walioitwa kwenye usaili INEC – NEC Tume ya uchaguzi Tanzania
Aidha, katika usaili unatakiwa kufanya yafuatayo:-
1. Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.
2. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha NIDA, Kitambulisho cha Mpira kura, Kitambulisho cha Mkazi, Hati ya Kusafiria, Leseni ya Udereva na Barua ya Utambulisho toka Serikali ya Kijiji kutoka kwa Mtendaji wa Kijiji, kwa watumishi wa Umma awe na kitambulisho cha kazi.
3. Kila msailiwa atajigharamia Chakula, Usafiri na Malazi.
4. Kila msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
5. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili ifahamike kuwa hakufanikiwa kuingia kwenye usaili.
6. Orodha ya waoitwa kwenye usaili imeambatanishwa na tangazo hili