Leo kutoka Sekretarieti ya Ajira Serikalini wametangaza fursa mpya pia, ajira mpya katika Nafasi za kazi Wilaya ya Rungwe – Utumishi Julai 2024. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe amepokea kibali cha Ajira Mpya kwa Ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chenye Kumb. Namba FA.97/288/01/09 ya tarehe 25/06/2024. Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:
Ajira Mpya Rungwe
1. DEREVA II – NAFASI 4
2. MWANDISHI MWENDESHA OFISI II – NAFASI 4
3. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II- NAFASI 8
4. MTENDAJI WA KIJIJI III – NAFASI 20
.Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na Vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
Ajira Mpya Rungwe 2024
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 04 Agosti, 2024
.MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE
S. L. P 148
RUNGWE