Leo, Sekretarieti ya ajira imetangaza ajira mpya au Nafasi za Kazi Manispaa ya Tabora – Utumishi Agosti 2024. Mkurugenzi wa Manispaa amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2023/2024 chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kufuatia kibali hicho Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora anakaribisha maombi kwa watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi zifuatazo :-
Ajira Mpya Manispaa ya Tabora
1. DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 05)
2. MTENDAJI WA MTAA lll – NAFASI (05)
3. MTENDAJI WA KIJIJI III – NAFASI TANO (05)
AJIRA MPYA MANISPAA YA TABORA
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 03 Septemba, 2024
MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi wa Manispaa,
Halmashauri ya Manispaa ya Tabora,
Mtaa wa Ikulu,
4Barabara ya Kiwanja cha Ndege,
S.L.P 174,
45182 TABORA.