Je, unatafuta matokeo ya usaili kwa ajira za Utumishi wa Umma mwaka 2024? Matokeo ya Usaili Utumishi (PSRS) – 2024 PDF, Hii ni fursa yako ya kupata taarifa muhimu na za uhakika kuhusu matokeo ya usaili ya mwaka huu kwa halmashauri mbalimbali nchini. Pia, soma zaidi kuhusu Jinsi ya Kuomba Kazi Utumishi hatua kwa hatua.
Tunakuletea matokeo haya kwa njia rahisi na inayopatikana kwa urahisi kupitia PDF, ikikupa nafasi ya kuangalia na kuchambua majina ya waliofaulu katika usaili.
Ajira Portal chaneli | Jiunge hapa |
Matokeo ya Usaili Utumishi, Hii ni hatua muhimu kuelekea ndoto yako ya kujiunga na Utumishi wa Umma, na tuko hapa kuhakikisha unapata taarifa zote unazohitaji kwa wakati unaofaa. Karibu uchunguze matokeo yako na ujue kama umepata nafasi unayoitarajia!
Matokeo ya Usaili Utumishi – Mambo ya kuzingatia
- Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapousaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
- Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
- Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
- Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
- Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
- Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
- Kila msailiwa atajigharamia chakula, usafiri na malazi.
- Kila msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
- Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa naMamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
- Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
- Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
- Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili
- Wasailiwa wote mnajulishwa kuwa hali ya hewa ya Jiji la Dodoma ni baridi hivyo mnashauriwa kuvaa nguo zinazohimili hali ya hewa ya ubaridi.
Matokeo ya Usaili Utumishi (PSRS) – Vitu vya Kuzingatia
Sasa Matokeo ya Usaili PSRS, Wasailiwa waliochaguliwa (SELECTED) kuendelea na usaili wanatakiwa kuzingatia muda na sehemu ya kufanyia usaili kama ilivyoainishwa kwenye tangazo la kuitwa kwenye usaili.
- Wasailiwa wote wanatakiwa kufika wakiwa wamevaa Barakoa (MASK)
- Wasailiwa wote wanakumbushwa kufika na vyeti vyao halisi (Original Certificates)
- Wasailiwa wote wanatakiwa kufika na vitambulisho vyao.
Matokeo ya Usaili wa kuandika Utumishi (PSRS)
2# Matokeo ya Usaili Ngara
Jinsi ya Kuomba Kazi Utumishi (PSRS)
- Mwombaji anapaswa kuunda akaunti kwenye tovuti ya ajira na kuiwezesha.
- Mwombaji anapaswa kusoma na kuelewa tangazo kabla ya kuomba kazi.
- Waombaji wanapaswa kuonyesha nafasi wanayoomba kwenye kichwa cha barua ya maombi.
- Mwombaji anakumbushwa kuambatanisha nyaraka zote muhimu (vyeti vya kitaaluma).
- Wasilisha barua yako ya maombi na utajulishwa juu ya mafanikio au kushindwa kwa maombi yako.
Bonyeza hapa kutuma na kuomba kazi Utumishi au Bonyeza hapa kuona matangazo ya nafasi za kazi mbalimbali kutoka PSRS.
Soma zaidi:
Leave a comment