Mwaka wa masomo wa 2024-2025 umewadia na pamoja nao matokeo muhimu ya uteuzi wa vyuo vya Afya na Sayansi Shirikishi kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET). Kwa wanafunzi na wazazi, habari hizi zimekuwa zikisubiriwa kwa hamu kubwa kwani zinatoa mwongozo wa mustakabali wa taaluma na maisha ya vijana wengi nchini. NACTVET Matokeo ya Waliochaguliwa Vyuo vya Afya na Sayansi Shirikishi 2024-2025 Vyuo vya afya 2024/25, kujiunga na vyuo, vyuo vya afya 2024, vyuo vya afya, nacte selections za vyuo vya afya, selection vyuo vya afya, majina ya waliochaguliwa kozi za afya, CAS Selection 2024,
Matokeo ya waliochaguliwa vyuo vya Afya, yanaakisi juhudi na bidii ya wanafunzi, pamoja na dhamira ya NACTVET ya kuhakikisha ubora wa elimu na mafunzo kwa ajili ya kuendeleza sekta muhimu za afya na sayansi shirikishi. Katika makala hii, tutachambua kwa kina matokeo haya, tukieleza mchakato wa uteuzi, vyuo vilivyopata nafasi za juu, na fursa zilizopo kwa wale waliochaguliwa. Karibu tujifunze zaidi kuhusu safari hii muhimu ya kielimu na hatua zinazofuata kwa wanafunzi wa mwaka huu.
Ajira Portal chaneli | Jiunge hapa |
Matokeo ya Waliochaguliwa Vyuo vya Afya 2024
Selection vyuo vya afya, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linautangazia umma matokeo ya uchaguzi wa awamu ya kwanza kwa walioomba kujiunga na programu za Afya na Sayansi Shirikishi kwa mwaka wa masomo 2024/2025.
Waliochaguliwa kozi za Afya, Jumla ya waombaji 24,629 waliwasilisha maombi yao kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS). Waombaji 23,503 walikamilisha maombi yao kwa kuchagua vyuo/programu walizozipenda. Waombaji 21,661 walikuwa na sifa kwenye programu walizoomba na waombaji 1,842 hawakuwa na sifa kwenye programu walizoomba.
CAS Selection 2024, Jumla ya waombaji 16,646 wamechaguliwa kujiunga kwenye vyuo 221 vinavyotoa programu mbalimbali za Afya na Sayansi Shirikishi ambapo wanawake 8,821 (53%) na wanaume 7,825 (47%).
Aidha, waombaji wenye sifa ambao hawakuchaguliwa kutokana na ushindani katika programu na vyuo walivyoomba wanashauriwa kuomba kujiunga katika programu na vyuo vyenye nafasi katika dirisha la awamu ya pili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja.
NECTA Matokeo ya waliochaguliwa kujiunga na kozi za Afya 2024
Waombaji wote wanaweza kuangalia matokeo ya uchaguzi kupitia tovuti ya Baraza (www.nactvet.go.tz) kwa kubonyeza CAS Selection 2024 kwa ajili ya kupata taarifa zaidi.
Aidha, Baraza linautaarifu umma kuwa dirisha la awamu ya pili limefunguliwa rasmi leo tarehe 11/07/2024 na litakuwa wazi hadi tarehe 10/08/2024, matokeo ya uchaguzi yatatolewa tarehe 16/08/2024.
Tangazo la NACTVET MATOKEO YA UDAHILI WA VYUO VYA AFYA AWAMU YA KWANZA
CAS Selection 2024
Mwaka wa masomo wa 2024-2025 unaleta fursa mpya kwa wanafunzi waliotuma maombi ya kujiunga na vyuo vya afya kupitia Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET). Matokeo ya udahili yamekuwa yakisubiriwa kwa hamu na wanafunzi pamoja na wazazi wao, kwani yanatoa mwelekeo wa kitaaluma kwa wanafunzi wengi.
Ili kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anaweza kufikia matokeo yake kwa urahisi, NACTVET imeweka mfumo mzuri wa mtandaoni. Hapa chini ni hatua za kuangalia matokeo ya udahili:
Jinsi ya kuangalia Matokeo ya waliochaguliwa Vyuo vya Afya NACTVET – NECTA
- Tembelea Tovuti Rasmi ya NACTVET: Anza kwa kufungua kivinjari chako na tembelea tovuti rasmi ya NACTVET kwa anwani ifuatayo: https://www.nactvet.go.tz/.
- Nenda kwenye Sehemu ya Matokeo “CAS Selection 2024”: Mara baada ya kufika kwenye ukurasa wa kwanza wa tovuti, tafuta na bofya sehemu iliyoandikwa ‘Matokeo ya Udahili‘.
- Chagua Mwaka wa Masomo: Katika ukurasa wa matokeo, chagua mwaka wa masomo 2024-2025 ili kupata matokeo ya sasa.
- Weka Taarifa Zako: Weka taarifa zako binafsi kama vile namba ya udahili au jina lako kamili katika sehemu husika.
- Bofya Kitufe cha Kutafuta: Baada ya kuweka taarifa zako, bofya kitufe cha ‘Tafuta’ au ‘Search’ ili kuona matokeo yako.
- Pakua na Kuchapisha: Ukishapata matokeo yako, unaweza kuyapakua na kuyachapisha kwa ajili ya kumbukumbu na hatua zaidi.
Soma zaidi: Nafasi za kazi Wilaya ya Tanganyika – July 2024
Leave a comment