Leo julai 9, 2024, Jiji la Arusha limetangaza nafasi mpya, Nafasi 55 za Ajira Kutoka Jiji la Arusha ambazo zimezua hamasa kubwa miongoni mwa wakazi na vijana wa mji huo. Fursa hizi zinawapatia wananchi nafasi adimu ya kujenga maisha bora na kuchangia katika maendeleo ya jamii yao.
Ajira mpya Arusha, Kutoka kwa sekta mbalimbali kama vile afya, elimu, na utawala, nafasi hizi za ajira ni mlango wazi kwa wale wenye bidii na ari ya kufanya kazi kwa kujituma na kuleta mabadiliko chanya katika Jiji la Arusha. Hii ni nafasi ya pekee ya kukamata hatma yako ya kimaisha na kitaaluma, na kuchangia katika ujenzi wa taifa letu.
Ajira Portal chaneli | Jiunge hapa |
Nafasi za kazi Arusha, Kwa mujibu wa kibali cha ajira mpya chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, anawatangazia wananchi wote Raia wa Tanzania kuomba nafasi za Kazi zifuatazo:-
Nafasi za kazi Jiji la Arusha
1. Dereva Daraja la II – Nafasi 7
Sifa za Mwombaji:
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI), Awe na Leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Cource) yanayotolewa na chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine kinachotambulika na Serikali
Majukumu:
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari na vi. Kufanya usafi wa gari
Ngazi ya Mshahara:
- Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B
2. Mtendaji wa Mtaa III – Nafasi 40
Sifa za Mwombaji:
Kuajirwa mwenye Elimu ya Kidato cha cha Nne (IV) au sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Chuo chochote kinachotambulika na Serikali.
Majukumu ya Kazi:
- Katibu wa Kamati ya Mtaa ii. Mtendaji Mkuu wa Mtaa
- Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika Mtaa.
- Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Mtaa
- Msimamizi wa Utekelezaji wa Sheria Ndogo pamoja na Sheria nyingine zinazotumika katika Mtaa
- Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama.
- Msimamzi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na umaskini katika Mtaa
- Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi wote
- Kuandaa na kutunza rejesta ya wakazi wote wa Mataa na x. Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata
Mshahara:
- Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B
3. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 3
Sifa za Mwombaji:
- Kuajiriwa Wahitimu wa kidato cha Nne (IV) wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili. Aidha, wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata program za komputa za ofisi kama vile: Word, Excel, Powerpoint, Internet, E-mail and Publisher kutoka Chuo chochote kinachotambulika na Serikali
Majukumu ya kazi:
- Kuchapa barua , taarifa na nyaraka za kawaida ii. Kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
- Kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi
- Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika vi. Kukusanya, kutunza na kurejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi maandalizi ya vikao mbalimbali na viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi
Mshahara:
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C
4. Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – Nafasi 5
Sifa:
- Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI). Awe na Stashahada (NTA level 6) katika fani ya Masjala kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.
Majukumu:
- Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye regista (incoming correspondence register)
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi (outgoing correspondence register);
- Kusambaza majalada kwa watendaji (action officers) iv. Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji.
- Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/maja;lada yanayohitajika na watendaji,
- Kurudisha majalada kwenye shubbaka/kabati la majalada (racks/filing cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa. vii. Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (File tracking)
Ngazi ya mshahara. Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C
Ajira Mpya Jiji la Arusha
Pakua hapa Tangazo la nafasi za kazi Halmashauri ya Jiji la Arusha
Soma zaidi: Ratiba ya NEC (INEC) Tanzania 2024/2025
Leave a comment