Karibu kwenye ukurasa wa Nafasi za kazi Manispaa ya Ubungo – Julai 2024 – Ajira Mpya Ubungo! Manispaa ya Ubungo, inayojulikana kwa jitihada zake za kuimarisha huduma za kijamii na kiuchumi kwa wakazi wake, imefungua milango kwa nafasi mpya za ajira.
Ajira Mpya Ubungo, Hii ni fursa adhimu kwa wataalamu na wale wanaotafuta kazi kujiunga na timu yenye malengo makubwa ya kuboresha maisha ya watu wa Ubungo. Nafasi hizi ni sehemu ya mpango wa utumishi unaolenga kuongeza ufanisi na kutoa huduma bora kwa wananchi. Tunakukaribisha kupitia orodha ya nafasi hizi na kutuma maombi yako ili uweze kuwa sehemu ya mabadiliko chanya katika jamii yetu. Usikose nafasi hii muhimu ya kuwa sehemu ya maendeleo ya Ubungo!
Ajira Portal chaneli | Jiunge hapa |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo amepokea Kibali cha Ajira mpya kutoka kwa Katibu Mkuu OR – Utumishi chenye Kumb.Na. FA. 97/288/01/09 ya tarehe 25.6.2024. Hivyo anapenda kuwatangazia Watanzania DARAJA wote wenye sifa kutuma maombi kwa kada mbili (02) kama zilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa hapo chini: –
Nafasi zilizo Tangazwa
1. Mtendaji wa Mtaa Daraja la III – Nafasi 25
2. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 1
Jinsi ya kutuma Maombi
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kieletroniki wa Ajira kupitia anwani ifuatayo; Bonyeza Hapa (anwani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa (Recruitment Portal). Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 25 Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi wa Manispaa,
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo,
S.L.P 55068,
DAR ES SALAAM.
Leave a comment