Karibu kwenye ukurasa wetu maalum wa Nafasi za Kazi Wilaya ya Chunya – July 2024. Tunakuletea fursa za ajira mpya kutoka Chunya, wilaya yenye utajiri wa rasilimali na fursa mbalimbali za kiuchumi. Hapa, utapata taarifa muhimu kuhusu nafasi za kazi zinazopatikana, masharti ya kuomba, na maelekezo ya jinsi ya kuwasilisha maombi yako kwa mafanikio. Jiunge nasi katika safari ya kuboresha maisha yako kupitia ajira hizi adhimu na kufanya Chunya kuwa sehemu bora zaidi kwa maendeleo yako ya kiuchumi na kijamii. Usikose fursa hizi muhimu, bofya hapa kwa maelezo zaidi na uanze mchakato wa kuomba sasa!
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya amepokea kibali cha Ajira Mpya kwa Ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chenye Kumb. Namba FA.97/288/01/09 ya tarehe 25/06/2024. Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-
Nafasi zilizo Tangazwa
1. Dereva – Nafasi 1
2. Mwandishi Mwendesha Ofisi – Nafasi 2
3. Msaidizi wa Kumbukumbu – Nafasi 2
4. Mtendaji wa Kijiji – Nafasi 5
Soma zaidi: Nafasi za kazi NCBA Tanzania – July 2024
Jinsi ya Kutuma Moambi
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anauani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ . Anuani hii inapatikana pia kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 21 Julai, 2024.
Leave a comment