Karibu kwenye orodha ya nafasi za kazi za hivi punde katika Wilaya ya Nyang’hwale kwa mwezi Julai 2024. Nafasi za kazi Wilaya ya Nyanghwale – July 2024 – Ajira Mpya Nyanghwale, Fursa hizi mpya za ajira zinalenga kuimarisha uchumi wa jamii na kuwapa wakazi wa Nyang’hwale nafasi ya kuboresha maisha yao kupitia ajira zenye tija na malipo bora. Tafuta nafasi inayokufaa na jiunge na timu yenye nia ya kuboresha maendeleo ya eneo hili. Usikose nafasi hii muhimu ya kuwa sehemu ya mabadiliko chanya katika Wilaya ya Nyang’hwale!
Ajira Portal chaneli | Jiunge hapa |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang`hwale amepokea kibali cha Ajira mpya kutoka kwa Katibu Mkuu OR – Utumishi chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024. Hivyo anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa kada mbili (02) kama zilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa: –
Nafasi zilizo Tangazwa
1. Mwandishi Mwendesha Ofisi – Nafasi 2
- Kuajiriwa Wahitimu wa kidato cha Nne au sita wenye Stashahada(Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya uhazili. Aidha ,wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata programu za kompyuta za ofisi kama vile:Word,Excel ,Powerpoint ,internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
2. Msaidizi wa Kumbukumbu – Nafasi 2
- Awe na Elimu ya kidato cha Nne (Form IV) au cha sita (Form VI) aliehitimu mafunzo ya Stashahada /Diploma (NTA level 6) katika fani ya Masijala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali ,wenye ujuzi wa kompyuta.
Jinsi ya kutuma Maombi
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa ajira(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretariet ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 22 Julai, 2024.
Leave a comment