Karibu kwenye ukurasa wetu wa Nafasi za kazi Wilaya ya Tanganyika – July 2024 – Ajira Mpya Tanganyika. Wilaya ya Tanganyika inakuletea fursa nyingi za ajira mpya zinazohusisha sekta mbalimbali. Huu ni wakati wako wa kuchangamkia nafasi hizi za kipekee na kujiunga na timu ya watumishi wenye maono na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Kila nafasi imeambatana na maelezo kamili kuhusu vigezo na sifa zinazohitajika, kuhakikisha unapata nafasi bora inayokidhi malengo yako ya kitaaluma. Fuatilia hapa kwa matangazo ya ajira mpya na ujitayarishe kwa hatua inayofuata katika safari yako ya kikazi.
Ajira Portal chaneli | Jiunge hapa |
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika amepokea Kibali cha Ajra mpya kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia barua yenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 ya tarehe 25.06.2024. Hivyo, anawatangazia wananchi wote wenye sifa kuomba nafasi mbalimbali za kazi. Nafasi husika ni kama zifuatavyo; –
Nafasi zilizo Tangazwa
1. Dereva Daraja la II – Nafasi 3
2. Mwandishi Mwendesha Ofisi – Nafasi 4
3. Msaidizi wa kumbukumbu – Nafasi 3
4. Mtendaji wa kijiji – Nafasi 5
Jinsi ya kutuma Maombi
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kieletroniki wa Ajira kupitia anwani ifuatayo; Bonyeza Hapa (anwani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa (Recruitment Portal). Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 23 Julai, 2024.
Soma zaidi: Viwango vya Mishahara 2024-25 Serikalini
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika,
S.L.P. 1,
MPANDA.
Leave a comment