Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imechapisha orodha ya majina ya waombaji NEC Walioitwa kwenye Usaili Tume ya Uchaguzi INEC 2024 kwa ajili ya nafasi mbalimbali za kazi. Orodha hii inajumuisha wale waliokidhi vigezo vya awali na watakaoendelea na mchakato wa usaili. Walioitwa wanapaswa kuhakikisha wanazingatia tarehe, muda, na mahali pa kufanyia usaili kama ilivyotajwa kwenye tangazo rasmi. Kujua zaidi kuhusu majina ya walioitwa na maandalizi ya usaili, tafadhali endelea kusoma makala hii.
Ajira Portal Chaneli | Jiunge hapa |
Hivyo basi, Afisa mwandikishaji Jimbo la Tabora Mjini anapenda kuwajulisha kuwa, wafuatao wameitwa kwenye usaili wa nafasi za waandikishi wasaidizi na Waendesha Vifaa vya BVR KIT (OPERATOR) katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakaofanyika kwa siku Mbili katika Ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kuanzia Tarehe 11.07.2024 hadi 12.07.2024 kama inavyoelezea hapa chini:-
Walioitwa kwenye usaili NEC
KUNDI A: Kata za: Ikomwa, Kakola, Uyui, Kabila, Misha, Kalunde, Tumbi, Ntalikwa, Kanyenye, Malolo, Mwinyi, Itetemya, Kitete, Ng’ambo na Tambukareli. Waombaji kutoka kata tajwa hapo juu wanatakiwa kufika Tarehe 11.07.2024 saa 2:00 asubuhi katika Ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa Tabora kwa ajili ya Usaili.
KUNDI B: Kata za: Itonjanda, Ifucha, Ndevelwa, Mbugani, Gongoni, Kiloleni, Mapambano, Cheyo, Ipuli, Mpela, Mtendeni, K/Chekundu, Chemchem na Iseyeva. Waombaji kutoka kata tajwa hapo juu wanatakiwa kufika Tarehe 12.07.2024 saa 2:00 asubuhi katika Ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa Tabora kwa ajili ya Usaili.
Pamoja na Tangazo hili orodha ya majina ya waombaji yanapatikana kwenye mbao za matangazo kwa kila kata husika na tovuti ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ambayo ni http://www.taboramc.go.tz.
Majina ya walioitwa kwenye usaili NEC
1. Orodha ya walioitwa kwenye usaili INEC hapa
Nawatakia utekelezaji mwema.
Soma zaidi: Ajira 9483 za Afya Utumishi (PSRS) – Tamisemi 2024
Leave a comment