Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) ni chombo cha serikali chenye hadhi ya Idara inayojitegemea iliyoanzishwa mahususi kuwezesha mchakato wa kuajiri watumishi katika Utumishi wa Umma. yafuatayo ni maelezo yote kuhusu PSRS walioitwa kwenye usaili Tabora ambapo chini utaweka kupakua majina yote ya wanaotarajia kufanya usaili huo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 08.07.2024 hadi 10.07.2024 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:
- Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili. Muda na sehemu ambako usaili utafanyika umeainishwa kwa kila kada.
- Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa barakoa (mask).
- Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.
- Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na: Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga Kura, Kitambulisho cha Kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya Kusafiria.
- Wasailiwa wanatakiwa kufika na vyeti vyao halisi, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji.
- Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of Results, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form IV and form VI results slips) havitakubaliwa na hawataruhusiwa kuendelea na usaili.
- Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
- Kila msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
- Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania, wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA).
- Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
- Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na bodi zao za kitaaluma, wanapaswa kuja na vyeti vyao halisi vya usajili pamoja na leseni za kufanyia kazi.
- Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.
- Wasailiwa wote mnajulishwa kuwa hali ya hewa ya Manispaa ya Tabora ni baridi kwa sasa, hivyo mnashauriwa kuvaa nguo zinazohimili hali ya hewa ya ubaridi.
Bonyeza hapa kutazama majina ya walioitwa kwenye usaili Tabora.
Soma zaidi: Tanzania yapokea treni mpya za umeme kwa mtandao uliopanuliwa wa SGR
Leave a comment