Mwongozo: Ajira Mpya za Walimu Julai 2024 – Mfumo wa Maombi ya Ajira za Ualimu. Waombaji wa fursa za Ajira mnatakiwa kuhuisha (Update) taarifa zenu kwa kutumia namba ya utambulisho wa Taifa (NIN), kwenye eneo ya Personal Details, aidha mnatakiwa kuhuisha taarifa kwenye eneo la Academic Qualification kwa kuweka kozi yako kwenye Category husika. Ili kuona ‘STATUS’ ya maombi yako ya kazi, ingia sehemu ya ‘MY APPLICATION’ baada ya ku-‘login’ katika akaunti yako. Sehemu hii itakuwezesha kuona namba ya usaili kwa wale waliofanikiwa na sababu ya kutokuitwa kwa wale ambao hawajafanikiwa.
Mfumo wa Maombi ya Ajira za Walimu 2024
i. Unatakiwa kuingiza cheti kimoja kimoja katika mfumo bila ya kuvijumuisha eneo moja. (PDF)
ii. Wakati wa kuingiza taarifa za elimu ya sekondari kidato cha nne na sita hakikisha unaingiza namba sahihi (index number) iliyoko kwenye cheti cha kuhitimu.
iii. Endapo umesoma nje ya Tanzania unatakiwa kuweka barua ya uthibitisho kutoka Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa elimu ya sekondari na kwa elimu ya astashahada, stashahada uweke barua kutoka Mamlaka ya Elimu (NECTA) kwa waliomaliza Shahada nje ya nchi waweke nakala ya cheti cha Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).
Hakikisha umeingiza namba yako ya mtihani inayofahamika kama (index number) ukiainisha mwaka uliohitimu kwa usahihi na kisha bonyeza sehmu ya kuwasilisha (submit).
Baada ya kuwasilisha maombi, mfumo utaleta taarifa zako kutoka Baraza Mitihani na endapo utajiridhisha kuwa taarifa hizo ni sahihi, utathibitisha taarifa hizo kwa kubonyeza yehemu imeandikwa thibitisha na kuhifadhi (confirm and save).
Ajira za Walimu 2024
Maombi ya kazi: Taarifa ya kila hatua ya usaili mrejesho utaiona katika eneo hili na endapo utafaulu na kupangiwa kituo cha kazi, taarifa hizo zitaonekana katika eneo hili. Pia, ukifungua eneo hili na usione taarifa yoyote, tambua kuwa hujaomba kazi na unapaswa kuhakikisha taarifa zako zimejazwa vizuri na kurudia zoezi la kuomba kazi.
CV na Barua ya kazi Ajira za Ualimu – Walimu 2024.
Unaweza kuhariri barua yako ya maombi ya kazi kwa kuondoa uliyokuwa umeweka awali na kuweka barua nyingine. Utaweza kufanya hivi tu endapo bado tangazo la maombi ya kazi bado liko hewani na muda wa kuwasilisha maombi haujamalizika.
Baada ya kubonyeza kitufe cha kuhariri (edit) utatakiwa kuambatisha barua inayotakiwa na kubonyeza sehemu iliyoandikwa huisha (update) ili kuhifadhi (save) barua yenye mabadiliko katika mfumo.
Unaweza kutuma maombi ya kazi ZAIDI ya vituo VIWILI au zaid ya Mikoa miwili??
Maombi ya Kazi ya Ualimu: CV nzuri na mifano ya Barua.
Barua ya Maombi ya Kazi ya Ualimu: Zingatia tangazo husika linasemaje pia anuani kuweka sahihi yako uliyo isaini kwa mkono.
Mfano wa CV ya maombi ya kazi ya Ualimu: Zingatia uandishi mzuri kwa kufata mwongozo uliotolewa ili kujihepusha kukosa kazi au kukosa kutoitwa kazini au kwenye usaili.