TANGAZO LA KUJULISHWA KUHUDHURIA MAFUNZO YA UBORESHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Uchaguzi la Nkenge anapenda kuwataarifa wagwaniuaji walioorodheshwa katika jedwali hapo chini kuwa wamefaulu usaili na hivyo wanatakiwa kuhudhuria mafunzo ya kazi ya Waandikishi Wasaidizi na Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki kwa ajili ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura litakalofanyika tarehe 05 hadi 11 Agosti, 2024 katika Wilaya ya Missenyi.
MAMBO YA KUZINGATIA
- Mafunzo yatafanyika kuanzia tarehe 02 – 03 Agosti, 2024 saa 2:00 asubuhi.
- Kwa Tarafa ya Kiziba mafunzo yatafanyika katika Ukumbi wa shule ya Msngi Mugana B na Tarafa ya Missenyi mafunzo yatafanyika katika Ukumbi Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi.
- Kila mshiriki anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi, ambapo vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) sipo namba ya NIDA (NIN), Kitambulisho cha Mpiga Kura, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho toka kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji/Kata.
- Afisa Mwandikishaji Jimbo la Nkenge atagharimia posho ya mafunzo, Chakula na posho ya Usafiri kwa Washiriki waliokoawa mbali.
- Kila Mshiriki aingie tarehe, muda na mahali alipompangiwa kufanyia mafunzo. Aidha, Mshiriki atakayechelewa dakika 30 baada ya muda wa mafunzo kuanza hatapokelewa na nafasi yake atachukuliwa na miongoni mwa walio katika orodha ya usubiri.
Orodha ya wanaotakiwa kuhudhuria mafunzo imeambatishwa na Tangazo hili.
NEC Kuitwa kwenye mafuzo INEC 2024
Orodha ya majina ya mikoa mingine inapatikana katika tovuti husika. hivyo tembelea ili kuona jina lako.
Wap hamna