Baada ya kuainisha waombaji wahitaji na kuonesha taratibu makundi ya Kozi au programu zifuatazo zenye vipaumbele zitapewa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo Tanzania – HESLB kulingana na uwepo wa fedha.
Kundi la Kwanza:
Kozi katika kundi la kwanza ni: –
- Ualimu wa Sayansi (Fizikia, Kemia na Baiolojia), Ualimu wa Hisabati na TEHAMA;
- Sayansi za Afya (Udaktari, Upasuaji Meno, Madawa ya Mifugo, Ufamasia, Uuguzi, Ukunga, Shahada ya Sayansi katika Prosthetikia na Mifupa, Shahada ya Sayansi katika Mazoezi ya Viungo, Shahada ya Sayansi ya Afya na Maabara, Shahada ya Sayansi ya Maabara na Matibabu na Shahada ya Sayansi ya Teknolojia ya Mionzi;
- Programu za Uhandisi (Ujenzi, Mitambo, Umeme, Uchimbaji Madini, Utengenezaji Nguo, Kemikali na Usindikaji, Kilimo, Chakula na Usindikaji, Magari, Viwanda, Usafiri Majini, Teknolojia ya Uhandisi wa Baharini, Elektronikia na Mawasiliano, Usindikaji na Huduma baada ya Mavuno, Maji na Umwagiliaji, na Uhandisi wa Ndege;
- Jiolojia ya Petroli, Kemia ya Petroli; mafuta na gesi
- Kompyuta, Programu za Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mitandao,
- Takwimu Bima (Actuarial and Data sciences) Kilimo, Misitu, Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji.
KADA (KOZI) ZENYE KIPAUMBELE KUPATA MKOPO HESLB
Kundi la Tatu
(i) Programu katika kundi hili ni pamoja na Masomo ya Biashara na Uongozi, Sayansi za Jamii, Sanaa, Sheria, Lugha, Fasihi na Masomo ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano.
(ii) Programu nyingine zote ambazo hazijaorodheshwa katika kundi lolote kati ya hayo matatu, zitaangukia katika kundi la tatu.
KOZI ZENYE KIPAUMBELE KUPATA MKOPO HESLB
Kundi la Pili
Kozi katika kundi hili ni:
(i) Programu za Msingi za Sayansi (Shahada ya Sayansi kwa ujumla katika Wanyama, Mimea, Kemia, Fizikia, Baiolojia, Baiolojia ya Viumbe Vidogo, Baiolojia ya Mifugo na
Bioteknolojia, Uvuvi na Mifugo, Sayansi ya Mazingira na Uhifadhi, Matibabu, Hisabati na Takwimu, Sayansi ya Mazingira na Usimamizi, Afya na Mazingira, Baioteknolojia na Maabara, Wanyamapori na Uhifadhi, na Kompyuta); TEHAMA, Vipimo na Mizani, Mazingira na Maendeleo ya Miji.
(ii) Programu ya Sayansi ya Ardhi (Ubunifu Majengo, Ubunifu Mandhari nje ya Majengo, Usanifu ndani ya Majengo, Uchumi Ujenzi, Mipango Miji na Vijiji, Usimamizi na Uthaminishi Ardhi, Jiospasho, Teknolojia katika Usanifu).