Leo kutoka Utumishi (PSRS), Orodha ya majina ya walioitwa au Kuitwa Kazini Utumishi leo Julai 2024 yametangazwa. Hongera kwa walioitwa mnakaribisha kwenye Utumishi wa Umma, tunatarajia mtafanya kazi kwa bidii na weledi katika kuwatumikia Watanzania.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 10-06-2023 na tarehe 10-06-2024 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
Walioitwa kazini Utumishi Taasisi mbalimbali 2024
Orodha kamili ya majina ya walioitwa makazini ipo juu kwenye PDF.
Wanaokuja kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi wanapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi; Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, Kitambulisho cha Mpiga kura au Leseni ya Udereva.