Leo kutoka Sekretarieti ya ajira Utumishi (PSRS), Wametangaza Matokeo ya Usaili wa Kuandika TCAA – Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Julai 2024. Wasailiwa waliochaguliwa (SELECTED) kuendelea na usaili wanatakiwa kuzingatia muda na sehemu ya kufanyia usaili kama ilivyoainishwa kwenye tangazo la kuitwa kwenye usaili.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ilianzishwa kwa kutunga Sheria ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ya mwaka 2003 Sura ya 80 (R.E 2006) ili kudhibiti Sekta ya Usafiri wa Anga katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuhakikisha utekelezaji mzuri wa Viwango na Taratibu Zinazopendekezwa. SARPs) kama ilivyoainishwa katika Viambatisho vya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO). Mamlaka pia ina jukumu la kudhibiti kiuchumi shughuli za watu na taasisi zinazotoa huduma za usafiri wa anga na huduma za uwanja wa ndege. Zaidi ya hayo, Mamlaka inatoa huduma za usafiri wa anga katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na anga za juu za Rwanda na Burundi.
Matokeo ya Usaili TCAA
1. Wasailiwa wote wanatakiwa kufika wakiwa wamevaa Barakoa (MASK)
2. Wasailiwa wote wanakumbushwa kufika na vyeti vyao halisi (Original Certificates)
3. Wasailiwa wote wanatakiwa kufika na vitambulisho vyao.
Matokeo ya Interview Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) 2024.
Kwa walioitwa kwenye usaili TCAA mara ya kwanza basi matokeo yao ya mara ya pili yako tiari.
Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti ya sekretarieti ya ajira Utumishi.