Leo kutoka Utumishi (PSRS), Pitia tangazo la ajira mpya Nafasi za kazi Mbozi – Utumishi Julai 2024; Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi amepokea kibali cha Ajira mpya kutoka kwa Katibu Mkuu OR – Utumishi chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024. Hivyo anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa kada tano (05) kama zilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa: –
Ajira Mpya Mbozi
1. MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 5
2. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II – NAFASI 2
3. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI 10
4. DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 4
5. MHUDUMU WA JIKONI – NAFASI 2
Bonyeza hapa kudownload tangazo la nafasi za kazi Mbozi
Endelea kusoma maelezo zaidi au kama una swali uliza hapo chini..
Ajira Mpya Mbozi – Nafasi za Halmashauri 2024.
Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30 Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 3,
MBOZI