Leo kutoka sekretarieti ya ajira (PSRS), Pitia tangazo la ajira mpya katika Nafasi za kazi Mji Tunduma – Utumishi Agosti 2024. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Mji Tunduma kuomba nafasi ya kazi iliyotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb Na. FA. 228/613/01/D/083 cha tarehe 25 Julai, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Ajira Mpya Tunduma
1. DEREVA DARAJA II (DRIVER II) – (NAFASI 1)
MAJUKUMU YA KAZI
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali; na
- Kufanya usafi wa gari
AJIRA MPYA TUNDUMA 2024 – AGOSTI UTUMISHI
Kuajiriwa mwenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na leseni Daraja āEā au āCā ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua Mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 19/08/2024.
Muhimu: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Mkurugenzi wa Mji,
Halmashauri ya Mji Tunduma,
S.L.P. 73,
TUNDUMA