Tanzania: Nafasi za Kazi Ukerewe – Utumishi Julai 2024; Kufuatia kutolewa kwa Kibali cha Ajira Mpya chenye Kumb Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe anawatangazia nafasi ya kazi Watanzania wenye sifa na uwezo ya kujaza nafasi tisa (9):-
Ajira Mpya Ukerewe
MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI TANO (5)
WASAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI (2)
DEREVA WA VIVUKO/MASHUA NAFASI (2)
Ajira Mpya Ukerewe – Nafasi za Halmashauri Julai 2024.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 26 Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe,
S. L.P. 41,
NANSIO/UKEREWE