Leo kutoka sekretarieti ya ajira (PSRS), Pitia tangazo la ajira mpya katika Nafasi za Kazi Wilaya ya Kilolo – Utumishi Julai 2024. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kuomba nafasi za kazi zilizotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb Na: FA.97/288/01”A”/2 cha tarehe 28 Mei, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Ajira Mpya Kilolo
1. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III- NAFASI 4
2. DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 3
3. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI 4
Ajira Mpya Kilolo 2024
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 12 Agosti, 2024
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya Kilolo,
S.L.P. 2324,
KILOLO.