Maelezo kuhusu Nafasi za kazi Wilaya ya Magu – Utumishi; Halmashauri ya Wilaya ya Magu imepokea kibali cha ajira mpya chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 chenye Kada ya Mtendaji wa Kijiji Daraja la III nafasi Ishirini na tano (25), Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II nafasi nane (08) na Dereva Daraja la II nafasi Tano (05) Msaidizi wa Kumbukumbu Nafasi tano (05) kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa watanzania wote wenye sifa na kuleta maombi ya kazi kwa nafasi zilizoainishwa hapo chini:
Nafasi zilizo tangazwa Magu
- MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI (25)
- DEREVA DARAJA LA II NAFASI TANO (05)
- MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II NAFASI NANE (8)
- MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI TANO (05)
Bonyeza hapa kudownload tangazo au hapa kutuma maombi yako katika nafasi za kazi zilizo tangazwa magu.
Endelea kusoma chini au uliza swali lako.. pia, pitia makala mbalimbali hapa habari times
Ajira Mpya Wilaya ya Magu 2024
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 28 Julai, 2024
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA
S.L.P. 200
MAGU