Leo kutoka sekretarieti ya ajira (PSRS), Pitia tangazo la ajira mpya katika Nafasi za Kazi Wilaya ya Mbeya – Utumishi Julai 2024. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya amepokea kibali cha Ajira Mpya kwa Ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chenye Kumb. Namba FA.97/288/01/09 ya tarehe 25/06/2024. Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:

Ajira Mpya Mbeya
1. DEREVA DARAJA II- NAFASI 2
2. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI 5
3. MWANDISHI MWENDESHA OFISI II – NAFASI 3
4. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II- NAFASI 5
Ajira Mpya Mbeya 2024
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 04 Agosti, 2024
MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi wa Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya,
S. L. P 599,
MBEYA.