Leo kutoka PSRS Sekretarieti ya Ajira, Serikali imetangaza Nafasi za kazi Wilaya ya Simanjiro – Utumishi Agosti 2024. Mkurugenzi amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2023/2024 chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kufuatia kibali hicho Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro anakaribisha maombi kwa watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi zifuatazo :-
Ajira Mpya Simanjiro
1. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II NAFASI 3
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini – Serikalini.
Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Ajira Mpya Simanjiro Agosti 2024
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 14 Agosti, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro,
S.L.P 9596,
ORKESUMET.