Leo kutoka Utumishi (PSRS), Wametangaza Ajira Mpya Nafasi za kazi Wilaya ya Singida – Utumishi Julai 2024; Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024. Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-
Ajira Mpya Singida
1. DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 02
2. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 03
Bonyeza hapa kudownload Tangazo la nafasi za kazi Singida
Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
Endelea kusoma maelezo mengine yote hapo chini..
Ajira Mpya Singida – Nafasi za Halmashauri 2024
Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 01 Agosti, 2024
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –
Mkurugenzi wa Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 27,
SINGIDA.