Nafasi za kazi JWTZ 2024, Kujiunga na Jeshi la wananchi Tanzania Nafasi za Kujiunga na Jeshi 2024 JWTZ Tanzania Uwandikishaji wa Vijana kwa Watanzania wenye nia na sifa zilizo tajwa hapa chini.
TANGAZO LA NAFASI ZA JESHINI 2024
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
Utaratibu wa kutuma maombi ni ufuatao:
1#. Kwa vijana waliopo katika makambi ya JKT ‘Operesheni Jenerali Venance Mabeyo’ taratibu zao zinratibiwa na Makao Makuu ya Jeshi.
2#. Kwa vijana waliopo nje ya Makambi ya JKT, maombi yao yaandikwe kwa mkono na kuwasilishwa Makao Makuu ya Jeshi Dodoma kuanzia tarehe 01 Agosti, 2024 hadi tarehe 14 Agosti, 2024 yakiwa na viambatisho vifuatavyo:
(1) Nakala ya kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA.
(2) Nakala ya cheti cha kuzaliwa.
(3) Nakala za vyeti vya shule.
(4) Nakala ya cheti cha JKT.
(5) Nambari ya simu ya mkononi ya mwombaji.
MAOMBI YATUMWE KWA ANUANI IFUATAYO
Mkuu wa Utumishi Jeshini,
Makao Makuu ya Jeshi,
Sanduku la Posta 194,
DODOMA, Tanzania
kwa maelezo zaidi tembelea SUMA JKT kwenye ukurasa wao wa Instagramu.
Utaratibu wa Kujiunga na jeshi JWTZ 2024 / 2025
Askari atapewa nambari ya utumishi baada ya kufaulu mafunzo ya awali.
Atalitumikia Jeshi kwa kipindi cha mwanzo cha miaka sita, baada ya hapo atafanya kazi kwa mkataba wa miaka miwili miwili kwa kibali cha Mkuu wa Majeshi.
Kwa maelezo mengine tembelea tovuti ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
Jinsi ya kutuma maombi ya Ajira za Jeshi 2024.
Maombi yanatumwa kwa njia ya posta
MAOMBI YATUMWE KWA ANUANI IFUATAYO
Mkuu wa Utumishi Jeshini,
Makao Makuu ya Jeshi,
Sanduku la Posta 194,
DODOMA, Tanzania
Kuwa makini.
Unatumaje mm cjaelewa namba ya kutuma maombi au wana Link ya kutuma maombi
SIfa za Kujiunga na Jeshi la JWTZ Tanzania JESHI LA WANANCHI 2024
Mtu yeyote ataandikishwa kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa sifa zifuatazo: –
1. Awe raia wa Tanzania
2. Awe na Elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe amefaulu..
3. Awe hajaoa/hajaolewa
4. Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25
5. Awe na tabia na mwenendo mzuri
6. Awe na akili timamu na afya nzuri
Maombi hatuwezi kutuma kwa njia ya mtandao maana sisi wengine tunakaa vijijini uku Zanzibar
Na mtu ambae hajapitia JKT kwenye kutuma maombi inakuwaje
Je kama sina kigezo cha JKT naruhusiea kutuma maombi
Mshahara wa Mwanajeshi 2024/2025
Naomba kujua kiwango cha mshahara wa mwanajeshi wa Tanzania ni kiasi gani