Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mkataba kutoka Wilaya ya Muleba 2025 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba anawatangazia nafasi za kazi watanzania wote wenye sifa za kuajiriwa katika nafasi ya Mwandishi wa Habari wa Redio, Fundi Mitambo Msaidizi na Mzalishaji wa vipindi/Mtengeneza Maudhui Msaidizi. Hii ni kwa kuzingatia kibali cha Ajira ya muda kilichotolewa na Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango cha tarehe 23/04/2025.
