Kama wewe ni mwomba ajira katika Sekretarieti ya Ajira katika OR-Utumishi wa Umma, Basi hizi ndizo Sifa za Afisa Ununuzi Katika Ajira Utumishi.
Afisa Ununuzi ni mtaalamu anayehusika na mchakato wa manunuzi ndani ya serikali, shirika au kampuni. Majukumu yake ni pamoja na kutafuta na kuchagua wasambazaji bora, kujadiliana bei na masharti ya ununuzi, na kuhakikisha kuwa bidhaa na huduma zinazohitajika zinapatikana kwa wakati na kwa gharama nafuu. Afisa Ununuzi pia anasimamia mikataba na kuhakikisha kuwa masharti yote yanazingatiwa, pamoja na kudumisha rekodi za manunuzi kwa ajili ya uwazi na ufuatiliaji.
Mbali na hayo, Afisa Ununuzi anahakikisha kuwa michakato ya ununuzi inafuata sera na taratibu za serikali au shirika, na pia anahusika na kutathmini ubora wa bidhaa na huduma zinazopatikana. Kwa kufanya hivyo, wanasaidia katika kudhibiti gharama za uendeshaji na kuongeza ufanisi wa shughuli za shirika. Wanafanya kazi kwa karibu na idara nyingine kama vile fedha, utawala, na uzalishaji ili kuhakikisha kwamba mahitaji yote ya vifaa na huduma yanatimizwa kwa wakati muafaka na kwa viwango vinavyokubalika.
Sifa: Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza/Stashahada ya Juu ya Ununuzi na Ugavi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali AU wenye “Professional level Ill” inayotolewa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi nchini (Procurement and Supplies Professionals and Technicians Board – (PSPTB); au sifa nyingine inayolingana na hiyo inayotambuliwa na PSPTB na awe aliyesajiliwa na PSPTB kama “Graduate Procurement and Supplies Professional”.
Mshahara wa Afisa Ununuzi au Ugavi 2024/2025
Ni upi mshahara wa mtu aliesomea Maswala ya Afisa Ununuzi?
Ngazi ya mshahara ni TGS D yaani Tshs. .510,000.00 na kuendelea kwa kila mwezi. Hii hulipwa kwa kulingana na Elimu.