Kama wewe ni mwomba ajira katika Sekretarieti ya Ajira katika OR-Utumishi wa Umma, Basi hizi ndizo Sifa za Dereva Katika Ajira Utumishi.
Dereva ni mtu anayehusika na kazi ya kuendesha vyombo vya usafiri kama vile magari, malori, mabasi, au magari madogo ya kibinafsi au ya kibiashara. Katika ajira, dereva ana jukumu la kuhakikisha usafirishaji salama wa abiria, mizigo, au huduma maalum kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa kufuata sheria na kanuni za barabarani. Pia, dereva anatakiwa kudumisha hali nzuri ya gari kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na matengenezo madogo madogo kama vile kuangalia mafuta, breki, na tairi.
Mbali na hayo, dereva anapaswa kuwa na ujuzi wa kuzingatia ratiba na ramani za barabara, kuwa na uwezo wa kushughulikia hali za dharura barabarani, na kuwa na tabia nzuri na wateja au abiria. Katika mazingira ya kibiashara, dereva anaweza kuwa sehemu muhimu ya timu ya usafirishaji na kutoa mchango mkubwa katika kuhakikisha ufanisi na uaminifu wa huduma za usafiri zinatolewa kwa wakati na kwa usalama.
Sifa: Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
Mshahara wa Dereva 2024/2025
Ni upi mshahara wa mtu aliesomea Maswala ya Udereva?
Ngazi ya mshahara ni TGS B yaani Tshs. .450,000.00 na kuendelea kwa kila mwezi.
Kwa majina naitwa mike Anderson, Nina miaka 29, elimu ya form 4, ninaomba kazi ya udereva
0718205547/0623151894