Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinapenda kuwajulisha wanafunzi wote waliochaguliwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kujiunga chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) katika matawi yake yote (Dar-es-Salaam Campus, Mwanza Campus, Dodoma Campus na Simiyu Campus) kutembelea tovuti ya chuo: https://ems.ifm.ac.tz/application, ili kupata maelekezo namna ya kuthibitisha nafasi zao za kujiunga. Masomo yataanza mwezi wa kumi (Oktoba) endapo kutakuwa na mabadiliko ya tarehe ya kuanza masomo mtajulishwa.
Nyaraka za kujiunga na chuo zitapatikana kupitia akaunti ya mwanafunzi husika mara baada ya kuthibitisha nafasi yake. Wanafunzi hawa wamechaguliwa moja kwa moja, hivyo hawatakiwi kufanya maombi mapya bali kudhibitisha nafasi zao kupitia mfumo wa chuo wa maombi.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na ofisi ya udahili wa wanafunzi kupitia namba za simu zifuatazo.
PDF ya majina ya waliochaguliwa IFM ipo chini.
IFM Huduma kwa wateja
DAR ES SALAAM: +255-734-205030 / +255-734-205029 / +255-734-205028
MWANZA: +255-734-205026
DODOMA: +255-734-205025
SIMIYU: +255-734-205027
Orodha ya waliochaguliwa IFM Bonyeza Hapa – https://ifm.ac.tz/advertisements