Taasisi inayosimamia masuala ya usajili wa vizazi, vifo, ndoa, talaka, na udhamini nchini Tanzania ni wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA). RITA, ambao unalenga kurahisisha na kuboresha huduma za uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa na vifo, mfumo wa kidijitali unaoitwa eRITA. Kupitia eRITA, watumiaji wanaweza kuhakiki vyeti vyao bila kulazimika kutembelea ofisi za RITA moja kwa moja. Ufanisi na kupunguza muda wa kusubiri majibu, kuleta ufanisi na kupunguza fursa ya kufuatilia na kuthibitisha, uhalali wa vyeti vya kuzaliwa na vifo kwa njia ya mtandao.
Katika mwongozo huu, utajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kujiandikisha, kuingia kwenye mfumo, na kuomba uhakiki wa cheti cha kuzaliwa kupitia eRITA, RITA Jinsi ya kuhakiki cheti cha kuzaliwa eRITA. Mfumo huu umebuniwa ili kuhakikisha taarifa zako zinalindwa na huduma inatolewa kwa usahihi na kwa wakati.
Muongozo wa Kuhakiki Vyeti vya Kuzaliwa na Vifo kwa Mfumo wa Kidijitali Kupitia eRITA
- Ingia kwenye tovuti ya Wakala https://www.rita.go.tz.
- Bonyeza kitufe kilichoandikwa eRITA kwenye ukurasa wa mwanzo.
- Chagua Huduma za Vizazi na Vifo.
- Bonyeza “Register“ katika kipengele cha usajili na jaza taarifa zote kwa usahihi ili kufungua akaunti yako (Muhimu: Nenosiri lazima liwe na herufi zaidi ya nane ikiwa na herufi kubwa, ndogo, namba, na alama yoyote mfano @#*&).
- Ingia katika akaunti yako ya barua pepe, fungua ujumbe ulio tumwa kutoka RITA, kisha bonyeza neno “Account Activation”.
- Baada ya kufungua akaunti, bonyeza “Sign In” na jaza taarifa sahihi ili kuingia katika mfumo.
- Chagua “Birth Services” kwa huduma za cheti cha kuzaliwa au “Death Services” kwa huduma za cheti cha kifo.
- Bonyeza “Request Verification” na jaza taarifa zote kwa usahihi.
- Chagua “Verification Reason”, ambapo uchague taasisi inayohitaji uhakiki mfano: LOANS BOARD, NHIF n.k.
- Ambatanisha cheti cha kuzaliwa/kifo kinachohakikiwa.
- Omba namba ya malipo kwa kubonyeza “Request Control Number”.
- Fanya malipo sahihi kulingana na ankara uliyopewa.
Kumbuka:
- Majibu ya uhakiki yatatumwa kupitia akaunti uliyofungua.
- Tunza nywila/nenosiri la akaunti uliyofungua.
- Ambatanisha kivuli (copy) katika mfumo wa PDF pamoja na taarifa zote ikiwa pamoja na namba ya ingizo (entry number) zinazohusika.
Soma zaidi: Nafasi za kazi Wilaya ya Buchosa – July 2024
Leave a comment