Ufadhili wa Samia (Samia Scholarship) 2024/2025 ni programu ya ufadhili maarufu inayotolewa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TAEC). Ufadhili huu umepewa jina kwa heshima ya Rais Samia Suluhu Hassan, na unalenga kusaidia wanafunzi bora nchini Tanzania ambao wanaonyesha ubora wa kitaaluma na uwezo wa uongozi.
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatekeleza mpango wa kukuza fani za Sayansi, Teknolojia, Ubunifu, Uhandisi, Hisabati na Tiba kupitia programu ya Ufadhili wa Samia (Samia Scholarship Extended Program).
Ajira Portal Chaneli | Jiunge hapa |
Wizara kupitia Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) inawatangazia Watanzania wenye Sifa kuomba ufadhili wa masomo ya Shahada za Juu (Uzamili) kwa wahitimu wenye ufaulu wa juu zaidi kwenye masomo ya sayansi kutoka katika vyuo vikuu vya Tanzania.
Nchi zinazolengwa
Ufadhili utatolewa kwa waombaji wenye udahili katika vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kwenye nchi zifuatazo: Australia, Austria, Ubelgiji, Kanada, China, Jamhuri ya Cheki, Finlandi, Ufaransa, India, Swideni, Korea ya Kusini, Urusi, Uturuki, Uingereza na Marekani.
Maeneo ya Ufadhili
- Sayansi na teknolojia ya nyuklia katika matibabu ya saratani (medical physics, nuclear medicine)
- Sayansi na teknolojia ya nyuklia katika utafiti wa maji, hewa na mimea (isotope hydrology, space/airborne technology)
- Sayansi na teknolojia ya nyuklia katika unururishaji wa vifaa tiba, bidhaa za viwandani na mazao.
- Sayansi na teknolojia ya nyuklia katika nishati ya nyuklia na utafiti wa vinu vya nyuklia na uzalishaji wa dawa za mionzi.
Soma zaidi: Jinsi ya kutuma maombi katika Mfumo wa Ajira Tume ya Utumishi wa Mahakama
Sifa za Mwombaji
- Awe Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 35;
- Awe mhitimu wa Chuo Kikuu katika shahada ya awali aliyemaliza katika kipindi kisichozidi miaka mitano kabla ya kuomba ufadhili huu.
- Awe na ufaulu wa juu wa kuanzia kiwango cha GPA ya 3.5 kati ya 5 au wastani wa ufaulu wa B kwa shahada ambazo hazina GPA kwenye matokeo ya jumla katika shahada ya awali ya sayansi, uhandisi, hisabati, tiba, tehama, mazingira, kilimo, na nishati pamoja na fani nyingine za vipaumbele vya Taifa;
Namna ya kutuma maombi
Muombaji anapaswa kujaza fomu maalumu inayopatikana katika mtandao wa TAEC kupitia kiunganishi hiki http://samiascholarship.taec.go.tz.
Leave a comment