Je, unatafuta kazi yenye hadhi, inayokuza taaluma yako na yenye mchango mkubwa kwa jamii? Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa inakuletea nafasi adimu za ajira kama Mtendaji wa Kijiji Daraja la III. Fursa hizi ni kwa Watanzania wenye sifa stahiki na ari ya kufanya kazi katika mazingira ya kipekee. Jiunge nasi na uwe sehemu ya maendeleo na ustawi wa kijiji! Usikose nafasi hii ya kipekee – tuma maombi yako sasa!
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa amepokea Kibali cha Ajira Mbadala kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia barua yenye Kumb. Na. FA.228/613/01/C/041 ya tarehe 21 Mei, 2024. Hivyo, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi zifuatazo:
Mtendaji wa Kijiji Daraja la III – Nafasi Mbili (2)
Sifa za Kuajiriwa:
Waombaji wanatakiwa wawe na Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form VI) na wawe wamehitimu astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii, au Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
Kazi na Majukumu ya Mtendaji wa Kijiji:
- Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji
- Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji
- Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
- Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini, na kuongeza uzalishaji mali
- Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalam katika kijiji
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji
- Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi
- Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za kijiji
- Atawajibika kwa Mtendaji Mkuu wa Kata
- Pamoja na kazi nyingine utakazopangiwa na Mwajiri wake
Mshahara: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B.
Jinsi ya Kuomba
Maombi yote yatumwe kwa njia ya barua pepe au kuletwa moja kwa moja ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 9 July 2024. Tafadhali hakikisha unaambatanisha vyeti vyote muhimu pamoja na barua ya maombi.
Soma zaidi: Jinsi ya Kujisajili/Kujiunga na Ajira Portal (Utumishi)
Leave a comment