Nafasi za kazi Manispaa ya Shinyanga; Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga amepokea Kibali cha Ajira Mpya kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia barua yenye Kumb.Na.FA. 97/288/01/09 ya tarehe 25 Juni, 2024. Hivyo; anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa watanzania wenye sifa za kujaza nafasi zifuatazo;-
Ajira Portal chaneli | Jiunge hapa |
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga inalenga kutoa huduma bora za kijamii na kiuchumi kwa wananchi kwa lengo la kufikia ukuaji endelevu wa uchumi na viwango vya mapato vinavyoendana na ongezeko la watu kwa kutumia fursa zilizopo ifikapo mwaka 2025
Nafasi zilizo Tangazwa
1. Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – Nafasi 4
2. Dereva Daraja la II – Nafasi 5
3. Mtendaji wa Mtaa Daraja la III – Nafasi 15
Jinsi ya kutuma Maombi
Maombi ya ajira katika tangazo la nafasi za kazi Kondoa yote yatumwe kwenye mfumo wa kieletroniki wa Ajira kupitia anwani ifuatayo; Bonyeza Hapa (anwani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa (Recruitment Portal). Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 25 Julai, 2024.
Leave a comment