Leo kutoka Utumishi (PSRS), Ajira Mpya – Nafasi za kazi Tume ya Utumishi Wa Bunge Tanzania – Utumishi Julai 2024; Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeundwa kwa mujibu wa Ibara ya 62 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977. Aidha, Ibara ya 88 ya Katiba inaunda Sekretarieti ya Bunge yenye jukumu la kuliwezesha Bunge kutekeleza majukumu yake. Kwa msingi huo, Sekretarieti ya Bunge, inatangaza nafasi za kazi za Kada mbalimbali ili kuimarisha utendaji wake. Watanzania wote wenye sifa na uwezo wanaalikwa kutuma maombi yao ili kujaza nafasi za kazi kama zilivyoainishwa hapa chini:-
Ajira Mpya Tume ya Utumishi wa Bunge
AFISA TAWALA DARAJA LA II – NAFASI 1: Kusimamia kazi za Utawala na Uendeshaji katika Taasisi;
FUNDI SANIFU DARAJA LA II (UMEME) – NAFASI 1: Kukagua na kuripoti kasoro za kiufundi za mifumo ya umeme.
FUNDI SANIFU DARAJA LA II (UFUNDI) – NAFASI 1: Kufanya ukaguzi wa ubora wa magari, mashine na mitambo na kushauri ipasavyo.
MTEKNOLOJIA DAWA DARAJA LA II – NAFASI 1: Kuainisha, kuandaa na kuagiza mahitaji ya dawa na vifaa tiba katika eneo lake la kazi;
TABIBU WA KINYWA NA MENO DARAJA LA II: Kutambua na kutibu magonjwa ya kawaida ya kinywa na meno.
Bonyeza hapa kudownload tangazo la nafasi za kazi Tume ya Utumishi wa Bunge
Hati za Matokeo za Kidato cha Nne na Sita HAZITAKUBALIWA.
Jinsi ya kutuma maombi katika nafasi za kazi Tume ya Utumishi wa Bunge 2024 Utumishi.
Maombi yote yatumwe kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: – https://portal.ajira.go.tz. (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa (Recruitment Portal). Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Ajira Mpya Tume ya Utumishi wa Bunge 2024.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 02 Agosti, 2024
MUHIMU
Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya
elimu. Barua hiyo ielekezwe kwa: –
KATIBU WA BUNGE
OFISI YA BUNGE
10 BARABARA YA MOROGORO
S.L.P. 941
40490 TAMBUKARELI
DODOMA.
Huduma kwa wateja Tume ya Utumishi wa Bunge Tanzania.
Kwa msaada na ufafanuzi piga namba; +255738685177. Simu zipigwe muda wa kazi kuanzia Saa 2:00 Asubuhi – 11:00 Jioni.
Limetolewa na: –
KATIBU WA BUNGE
OFISI YA BUNGE
DODOMA.