Hivi karibuni, Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetangaza nafasi za ajira mpya 9483 za Afya Utumishi (PSRS) – Tamisemi 2024 za sekta ya afya kwa mwaka 2024. Ajira hizi zinajumuisha nafasi mbalimbali kwa wataalamu wa afya, ikiwa ni pamoja na madaktari, wauguzi, na wataalamu wa maabara. Fursa hizi zinapatikana kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS). Hii ni nafasi muhimu kwa wataalamu wa afya wenye sifa za kitaaluma kutumikia jamii na kusaidia kuboresha huduma za afya nchini. Maombi yanakaribishwa kutoka kwa wote wenye vigezo vinavyohitajika, na ni matumaini yetu kuwa ajira hizi zitaleta mabadiliko chanya katika sekta ya afya nchini Tanzania.
Katibu wa Sekretarieti yaAjira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenyesifa na uwezo wa kujaza nafasi 9483 kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.
Ajira Portal Chaneli | Jiunge hapa |
Ajira za Afya Utumishi 2024 Masharti
- Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waombaji ambao tayari ni watumishi wa umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wajiridhishe ipasavyo.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha nne, kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika (Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates).
- – Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- – Computer Certificate
- – Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 20 Julai, 2024.
Nafasi za kazi Kada ya Afya Utumishi
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
KATIBU, OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.
Maombi yote yatume kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: Bonyeza Hapa.
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Soma zaidi: Ajira za Afya Utumishi (PSRS) 2024
Leave a comment