Katika mwezi wa Julai 2024, Manispaa ya Morogoro imefungua milango kwa Nafasi za Kazi Manispaa ya Morogoro – Julai 2024 – Ajira Mpya Morogoro, zenye lengo la kuimarisha utoaji wa huduma na kukuza maendeleo ya kijamii. Ajira hizi mpya ni fursa muhimu kwa wakazi wa Morogoro na maeneo jirani, kuwapa nafasi ya kuchangia katika kuboresha maisha ya jamii yao kupitia Utumishi. Jiunge na timu ya Manispaa ya Morogoro na uwe sehemu ya mabadiliko chanya kwa ajili ya mustakabali wa kizazi kijacho.
Ajira Portal chaneli | Jiunge hapa |
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 na Kibali cha Ajira mbadala chenye Kumb. Na. FA.228/613/01/C/042 cha tarehe 21 Mei, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi zifuatazo: –
Nafasi zilizo Tangazwa
1. Mtendaji wa Mtaa Daraja la II – Nafasi 22
- Sifa: Mwombaji awe na Cheti cha kidato cha nne/sita aliyehitimu mafunzo ya Astashahada / Cheti (NTA LEVEL 5) katika mojawapo ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka chuo cha Serikali za Mitaa au chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
2. Mwandishi Mwendesha Ofisi – Nafasi 1
- Sifa: Kuajiriwa mhitimu wa Kidato cha IV au Kidato cha VI wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na serikali. Awe 3 amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powepoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
Jinsi ya kutuma Maombi
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kieletroniki wa Ajira kupitia anwani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/advert/index (anwani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa (Recruitment Portal). Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 23 July, 2024.
Soma zaidi: Ajira Mpya 12000 za Walimu OR-Tamisemi
MUHIMU. Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa na ielekezwe kwa anuani ya;
Mkurugenzi,
Halmashauri ya Manispaa Morogoro,
S.L.P 166,
MOROGORO.
Leave a comment