Katika juhudi za kuboresha huduma kwa wananchi na kuimarisha utendaji kazi, Manispaa ya Temeke inatangaza Nafasi za kazi Manispaa ya Temeke – Julai 2024 – Ajira Mpya Temeke. Hizi ni ajira mpya ambazo zinatoa fursa kwa Watanzania wenye sifa zinazohitajika kujiunga na timu ya wataalamu wa Temeke. Nafasi hizi zinajumuisha nyanja mbalimbali, zikilenga kutoa huduma bora kwa wananchi na kuchangia katika maendeleo ya mkoa.
Ajira Mpya Temeke ni muhimu kwa wale wanaotafuta kazi zinazowiana na taaluma na uzoefu wao, huku wakipata nafasi ya kuchangia katika ujenzi wa jamii bora. Tafadhali soma maelezo ya nafasi hizi na taratibu za kuomba ili uweze kujipatia ajira yenye manufaa na yenye changamoto nzuri.
Ajira Portal chaneli | Jiunge hapa |
Hivyo basi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Manispaa ya Temeke kuomba nafasi za kazi ziliyotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Nafasi zilizo Tangazwa
1. Dereva Daraja la II – Nafasi 5
2. Mtendaji wa Mtaa – Nafasi 42
Jinsi ya kutuma Maombi
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kieletroniki wa Ajira kupitia anwani ifuatayo; Bonyeza Hapa (anwani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa (Recruitment Portal). Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 26 Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
MKURUGENZI WA MANISPAA,
HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE,
S. L. P 46343,
DAR ES SALAM.
Leave a comment