Leo tarehe 25/07/2024, Sekretarieti ya Ajira imetangaza nafasi za kazi iwe fursa mpya na Ajira Mpya Wilaya ya Mpimbwe – Utumishi Julai 2024. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024. Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-
Nafasi za kazi Mpimbwe
1. DEREVA II – NAFASI 03
2. MWANDISHI MWENDESHA OFISI II – NAFASI 01
3. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI 02
4. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III- NAFASI 06
Bonyeza hapa kudownload tangazo la nafasi za kazi Mpimbwe
Jinsi ya kutuma maombi utumishi maelezo yapo chini..
NAFASI ZA KAZI MPIMBWE JULAI 2024.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 07 Agost, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya Mpimbwe,
S.L.P. 245, MPANDA