Maelezo, Jinsi ya Kuomba Mkopo HESLB Bodi ya Mikopo Tanzania. Maombi yote ya mkopo yatafanyika kupitia Mfumo wa Maombi na Usimamizi wa Mikopo (OLAMS). Waombaji wote wa mikopo WANAKUMBUSHWA kutumia namba ileile ya Mtihani wa Kidato cha Nne iliyotumika wakati wanapoomba udahili vyuo.
Baada ya kukamilika kwa mchakato wa maombi kwenye mtandao, waombaji watapaswa kutoa nakala za fomu za mombi na mikataba ya mkopo kwenye mtandao, kugonga mihuri sehemu husika, kusaini fomu, kuambatanisha nyaraka zinazohitajika kwenye mtandao wa OLAMS kabla ya kutuma maombi hayo kwa njia ya EMS kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
HESLB House, 1 Mtaa wa Kilimo, Eneo la TAZARA,
S.L.P 76068,15471 Dar es salaam, TANZANIA.
Waombaji wanakumbushwa kutunza nakala ya fomu za maombi, viambatanisho vilivyowasilishwa na risiti ya EMS iliyotumiwa kutuma maombi yao kwa kufuatilia HESLB endapo itahitajika.
Mwisho wa kupokea maombi ya Mkopo / mikopo HESLB
A. Miongozo hiyo inapatikana kwenye tovuti yetu ya Bodi ya Mikopo ya http://www.heslb.go.tz toka Juni 01, 2024 na nawasihi waombaji mikopo kusoma na kuielewa miongozo hiyo kabla ya kuanza kufanya maombi ya mkopo, pamoja na kuzingatia muda uliopangwa wa kujaza maombi ya mkopo wa siku tisini (90), kuanzia Juni 01 hadi Agosti 31, 2024, amesisitiza Dkt. Kiwia.
Ada ya Maombi ya Mkopo HESLB (Bodi ya Mikopo Tanzania)
Waombaji wanapaswa kulipia ada ya maombi ya mkopo ya kiasi cha shilingi elfu thelathini (30,000) kupitia Benki ya NMB, CRDB au TPB au kwa mitandao ya simu ya M-PESA, TIGO PESA, na AIRTEL MONEY. Kwa maelezo zaidi tembelea: https:/olas.heslb.go.tz