Mwongozo: Usajili wa TIN au Jinsi ya Kupata TIN Namba TRA – Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). TIN, ambayo inasimama kwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi, ni namba ya utambulisho kwa ajili ya masuala ya kodi. Vifupisho vya jina kamili vinaweza kuwa na mchanganyiko wa namba au herufi. Nchi kadhaa za Afrika, ikiwemo Tanzania, zimeanza kutumia mfumo huu tangu ulipoanzishwa kwa mara ya kwanza nchini Marekani.
Jinsi ya Kupata TIN Namba Mtandaoni
Ili kupata TIN Number ya TRA mtandaoni, unapaswa kuwa na Namba ya NIDA. Mara baada ya kupata namba ya NIDA, ingia kwenye tovuti ya TRA ambayo ni: https://www.tra.go.tz Chagua Usajili wa TIN Mtandaoni Kisha fuata hatua nyingine kama inavyotakiwa, ni rahisi.
Aina Ngapi za TIN Namba Zipo Tanzania?
Hapa Tanzania kuna aina mbili za TIN ambazo ni namba za TIN za biashara na namba za TIN zisizo za biashara. Hii inamaanisha kama unataka kufanya biashara na unahitaji namba ya TIN utahitaji kuwa na namba ya TIN ya biashara.
Ikiwa mimi ninayo TIN tayari kuna haja ya kupata TIN Namba kwa ajili ya ajira?
Hapana TIN hiyo ya mwanzo ndio itatumika na TIN huwa ni moja kwa mtu mmoja.
TIN namba huitajika kwenye malipo gani?
Hutumika kwenye malipo ya kodi katika biashara, ajira, uwekezaji na pia katika malipo yasiyohusu kodi mfano ada ya leseni ya udereva.
Kuna matumizi ya aina ngapi ya TIN?
Kuna aina mbili ya matumizi ya TIN ambayo ni ya kibiashara na yasiyo ya kibiashara.
Nini maana ya TIN?
TIN ni namba ya utambulisho wa mlipakodi.