Ikumbukwe, Leo Utumishi (PSRS) walitoa tangazo la nafasi za ajira mpya za walimu (Ualimu) wa Watanzania wote wenye sifa. Hivyo huu ni mwongozo muhimu wa Jinsi Ya Kutuma Maombi Ajira Za Walimu (Ualimu) Utumishi – Ajira Portal 2024; Waombaji kazi wanatakiwa kuingiza namba sahihi zilizoko kwenye kitambulisho cha Taifa (NIDA).
Baada ya kuingiza namba hii, mfumo utawauliza maswali machache ili kuthibitisha umiliki wa namba hiyo. Ikithibitishwa kuwa ni sahihi, mfumo utaingiza moja kwa moja taarifa kutoka NIDA kwenye mfumo wa maombi ya kazi, kwa kufuata mwongozo uliotolewa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Mfumo wa maombi ya Ajira za Walimu 2024 Utumishi (Ajira Portal)
Kujisajili: Kama unataka kujisajili mwanzo kabisa wakati umeingia katika mfumo wa ajira basi Bonyeza Hapa.
Kufungua akaunti: Jinsi ya kufunfua akaunti utumishi (ajira portal) basi ni muhimu sana Bonyeza hapa kufungua.
Kutuma maombi: Jinsi ya kutuma maombi katika ajira za walimu 2024, Hii ni hatua muhimu sana baada ya kujaza taarifa zako zote muhimu katika sekretarieti ya ajira. Hivyo, unapaswa kuwa makini wakati wa ujazaji wa taarifa na nakala muhimu sana ili kuepusha makosa yatakayo jitokeza baada ya kukosea. Bonyeza Hapa kutuma maombi
Bonyeza hapa kudownload mwongozo mzima wa namna au jinsi ya kujisajili na mfumo
Baada ya taarifa zako kuingizwa kwenye mfumo wa ajira, unapaswa kumalizia kuingiza taarifa zote muhimu. Hakikisha umejaza taarifa binafsi kikamilifu na kisha bonyeza kitufe cha “Hifadhi” (Save) ili taarifa zako ziweze kuhifadhiwa kwenye mfumo na kuwa tayari kwa mchakato wa ajira.
Kumbuka: Hakikisha unajaza taarifa zako kwa umakini sana.
Mfumo wa Ajira za Ualimu Ajira Portal Utumishi 2024.
Jaza taarifa zote muhimu kwa kuzingatia mpangilio huu:
– Chagua ngazi yako ya Elimu
– Chagua nchi uliyosoma.
– Chagua fani sahihi kulingana na taaluma yako ili uweze jina sahihi la fani yako uliyohitimu.
– Chagua fani uliyofuzu na inatakiwa jina lake lifanane na kilichoandikwa kwenye cheti chako cha kuhitimu ambacho unataka kukiambatisha kwenye mfumo, endapo hujapata jina linaloendana na kozi uliyomaliza huenda umechagua sehemu isiyo sahihi na taaluma yako, hivyo tafuta sehemu nyingine kwa kutumia jina la fani uliyofuzu kama ilivyoandikwa kwenye cheti chako.
– Chagua au jaza jina la chuo na kama chuo ulichosoma hakipo andika jina kamili kwa kirefu, usitumie vifupisho havikubaliki.
– Onyesha ulianza lini na ulihitimu lini.
– Ambatisha nakala ya cheti kilichothibitishwa na mwanasheria na hakikisha cheti chako unachokiweka hakizidi 2MB.
– Bonyeza sehemu ya hifadhi (save) ili taarifa na nyaraka zako ziweze kuhuishwa na kuhifadhiwa kwenye mfumo.
Mfumo wa maombi ya ajira za walimu 2024 Utumishi.
Taarifa za Kitaaluma: Katika eneo hili, mwombaji wa ajira anapaswa kuchagua kiwango cha elimu kwenye eneo la “educational level”. Inashauriwa mwombaji kazi aanze na taarifa za kidato cha nne na kuendelea kulingana na kiwango chake cha elimu. Wakati wa kuingiza taarifa za kiwango cha elimu baada ya zile za elimu ya sekondari, mwombaji kazi anatakiwa kuchagua kundi la kozi yake (programme category).
Endapo umechagua kundi la kozi yako na usipoiona tambua kuwa hukuwa umechagua kundi stahiki na hivyo itakulazimu kurudi na kupitia makundi hayo upya. Aidha, kama mwombaji amesoma nje ya Tanzania atatakiwa kujaza kwenye eneo la kundi la kozi husika na Sekretarieti ya Ajira itathibitisha usahihi wa chaguo aliloliweka.