Ikumbukwe; Leo kupitia Wizara ya Afya wametangaza nafasi za Mafunzo ya Walimu (Ualimu). Hivyo huu ni mwongozo wa Jinsi ya Kutuma Maombi Mafunzo ya Ualimu 2024/2025 – MOEST TCMS Teacher Colleges Management System(TCMS) Student`s Portal. Wahitimu wa kidato cha nne, kidato cha sita na walimu waliohitimu Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi, wenye sifa zilizobaizinishwa katika tangazo hili wanaruhusiwa kutuma maombi;
Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Ualimu vya Serikali wanatakiwa kujisajili na kutuma maombi kielektroniki kupitia mfumo wa udahili wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia < – BOFYA HAPA KUJISAJILI ->.
Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu kwa vyuo visivyo vya Serikali watume maombi yao moja kwa moja katika vyuo wanavyotaka kusoma na vyuo husika viwasilishe sifa za waombaji Baraza la Mitihani Tanzania kwa uhakiki;
Mwombaji wa mafunzo ya Ualimu ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (Miaka 02) atachagua kozi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi;
Mwombaji wa mafunzo ya Ualimu ya Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) atachagua tahasusi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi;
Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali yatatolewa kwenye mfumo kupitia “account” aliyotumia mwombaji kuomba mafunzo ya Ualimu (kuanzia tarehe 25/08/2024) na katika Vyuo vya Ualimu walivyochaguliwa;
Fomu za kujiunga na Mafunzo zitatolewa kupitia tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (http://www.moe.go.tz) na Chuo atakachopangwa mwombaji kwa kutumia anuani yake. Waombaji wote wanashauriwa kuandika anuani kamili, barua pepe na namba ya simu inayopatikana kwa mawasiliano zaidi; na
Majibu na fomu za kujiunga na Chuo kwa watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu visivyo vya Serikali yatatolewa na vyuo husika.
Mfumo wa maombi ya mafunzo ya Ualimu 2024
Karibu kwenye Tovuti ya Wanafunzi ya TCMS. Kupitia tovuti hii utaweza kuomba kudahiliwa katika kozi mbalimbali zinazotolewa na Vyuo vya Ualimu, Kujiandikisha kwa ajili ya masomo katika kila muhula, Kuangalia matokeo ya mitihani na huduma nyinginezo binafsi.
Uchunguzi
Kwa uchunguzi wowote wa kutumia mfumo au mchakato wa udahili piga 0737 962 965 au tuma barua pepe kwa info@moe.go.tz