Majina ya Walioitwa Kazini Utumishi (PSRS); Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 10-06-2023 na tarehe 21-06-2024 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
Endelea kusoma hapo chini na tafta PDF ya majina ya walioitwa kazini kutoka Utumishi (PSRS)
Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenye Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala ya wazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili na baada ya hapo barua ambazo hazitachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.
Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira. Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.
Wengine tunaomba ila hatupati ajira tumechoka na maisha ya mitaani,,tulisomea kuteseka au kuajiriwa? Tumepoteza mda sana Bora nisingeenda shule tu,,
Endelea kuamini. Ipo siku utapata..
Wanaokuja kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi wanapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi; Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, Kitambulisho cha Mpiga kura au Leseni ya Udereva.
Pakua hapa orodha ya majina ya walioitwa kazini utumishi leo tarehe julai 15-2024
Bonyeza hapa – https://t.co/wzl7W50PZt