Waombaji mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2024/2025 wanafahamishwa kuzingatia mambo yafuatayo:
- Kusoma na kufuata taratibu za maombi katika Mwongozo huu wa mwaka wa masomo 2024/2024;
- Kuhakikisha kuwa namba ya mtihani wa kidato cha nne iwe sawa kwenye maombi ya mkopo na udahili wa chuo;
- Waombaji ambao wamefanya mitihani ya kidato cha nne zaidi ya mara moja wahakikishe wanaorodhesha namba zote katika maombi yao;
- Kuhakikisha kuwa nyaraka zote za maombi ya mkopo unazowasilisha ziwe zimehakikiwa na mamlaka husika;
- Kuhakikisha kwamba vyeti vyote vya kuzaliwa/vifo vinathibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) au wakala Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSRA) au Afisa aliyeteuliwa ili kuthibitisha uhalali huo;
- Kuhakikisha vyeti vyote vya kuzaliwa/vifo kwa Wanafunzi waliozaliwa nje ya nchi au wazazi waliofariki nje ya nchi vithibitishwe na ofisi za ubalozi husika zilizopo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
- Waombaji wajaze fomu zao kwa usahihi kabla ya kuziwasilisha;
- Maombi ya mikopo yanapaswa kuwa na taarifa sahihi na za kweli;
- Waombaji wote wanatakiwa kutunza nakala ya fomu ya maombi ya mkopo waliyowasilisha Bodi ya Mikopo kwa matumizi mengine (kama itahitajika);
Waombaji wote wanakumbushwa kuzingatia muda wa mwisho wa kutuma maombi.
MWONGOZO WA UTOAJI MIKOPO HESLB 2024/2025
i. Mwongozo wa Utoaji Mikopo HESLB kwa Wanafunzi wa Shahada ya Awali (Bachelor) kwa 2024 -2025,
ii. Mwongozo wa Utoaji Mikopo HESLB kwa Wanafunzi wa Stashahada (Diploma) kwa 2024 – 2025,
iii. Mwongozo wa Utoaji Mikopo HESLB kwa Stashahada ya Umahiri katika Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo kwa 2024 – 2025 (Post Graduate Diploma in Legal Practice),
iv. Mwongozo wa Utoaji Mikopo HESLB kwa Shahada za Umahiri na Uzamivu, na
v. Mwongozo wa Utoaji Ruzuku za Samia kwa mwaka 2024 – 2025